TANZANIA RED CROSS SOCIETY
Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania(TRCS) ni shirika la hiari la kibinadamu lililoanzishwa kama taasisi huru ya Kitaifa (National Society) kwa Sheria ya Bunge Na. 71 ya Disemba 1962 na kufanyiwa marekebisho na Bunge la Tanzania mwaka 2019. Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania kilitambuliwa na kukubaliwa uanachama wa Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC) mwaka 1963. Makao Makuu yapo Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Tanzania Red Cross Society anawatangazia vijana wa TRCS wenye sifa kujitokeza kugombea nafasi zifuatazo.