Rais wa Tanzania Red Cross Society Mhe. David M Kihenzile ametembelea Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu Mkoani Kigoma, ambapo Tanzania Red Cross Society linatoa huduma za afya kwa wakimbizi kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Katika ziara hiyo, Rais alifanya kikao na Siasa Manjenje Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu (Camp Commandant)na kujadili maendeleo ya utoaji wa huduma za Afya na changamoto zilizopo. Aidha, alitembelea idara ya wagonjwa wa nje (OPD), chumba cha upasuaji (Theatre), na famasi ili kujionea maendeleo ya mradi pamoja na mazingira ya kazi ya watumishi wa Red Cross.
Ziara hiyo ni sehemu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya Red Cross ambayo hufanywa na Katibu Mkuu wa Tanzania Red Cross Society Bi. Lucia Pande inayolenga kuboresha huduma za afya na ustawi wa wakimbizi kambini hapo.
Imetolewa Na:
Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano
Tanzania Red Cross Society















