Loading Events

Rais wa Turkish Red Crescent, Prof. Fatma Meric Yilmaz, leo amezindua mradi wa maji safi wilayani Mbinga, Jimbo la Mbinga Vijijini, unaojumuisha ujenzi wa visima vitano katika shule tatu za Msingi na Sekondari mbili. Shule hizo ni Mkako Sekondari, Shule ya Sekondari Mkumbi, Shule ya Msingi Maguu, Shule ya Msingi Lupilinga na Shule ya Msingi Mkwera. Gharama ya Mradi shilingi milioni 400 za kitanzania.

Uzinduzi huo ulifanyika katika Shule ya Sekondari Mkako, iliyopo katika Jimbo la Mbinga Vijijini, na ulihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Brig. Gen. Ahmed Abbas Ahmed, Balozi wa Uturuki Nchini Tanzania, Bekir Gezer, Mhe. Judith Kapinga ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo na Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhe. David Kihenzile (Mb) ambaye ni Rais wa Tanzania Red Cross na Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi,  Katibu Mkuu wa Tanzania Red Cross Society, Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Ruvuma na ya Wilaya ya Mbinga, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi, Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Idara, Sehemu na Vitengo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na Wananchi wanaoishi karibu na mradi huo.

Mkuu wa Mkoa Ruvuma, aliukaribisha ugeni wote Mkoani Ruvuma na kuishukuru sana Tanzania Red Cross Society na Turkish Red Crescent kwa msaada wa visima vitamin vya maji. Aliendelea kueleza kwamba bado mahitaji ya msaada katika Mkoa huo ni makubwa hivyo aliomba wadau hao kuendelea kuisaidia Ruvuma. Pia Mkuu wa Mkoa alimuomba Balozi kutangaza fursa za uwekezaji na za kitalii zilizopo katika Mkoa wa Ruvuma ili wafanyabiashara na watalii wamiminike kwa wingi Mkoani Ruvuma. Pia Mkuu wa Mkoa aliahidi kuwa mradi huo utalindwa kwa nguvu zote ili uwe wa kudumu.

Mhe. David Kihenzile, Rais wa TRCS, alimshukuru Prof. Fatma kwa kukubali kuja nchini na kuishukuru Turkish Red Crescent kwa ushirikiano wao wa miaka mingi, hasa katika kipindi cha Ramadhani na sikukuu za iddi, kwa misaada ambayo hutoa kwa watu wenye uhitaji. Alisema kuwa mradi huo ni mwanzo mzuri na endelevu kwa mustakabali wa vuguvugu la RCRC katika kusaidia jamii.

Mhe. Judith Kapinga alisema kuwa mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Serikali na ni hatua muhimu kuelekea kupatikana kwa maji safi kwa wananchi wa jimbo zima la Mbinga Vijijini. Aliwaahidi wananchi hao kuwa ataendelea kupambana kwa hali na mali kuhakikisha kuwa anawaletea maendeleo na anatimiza ahadi alizozitoa wakati wa kugombea